• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfumo wa ushirikiano wa pande tatu za China, Ujerumani na Afrika kusaidia kutimiza lengo la nishati endelevu la Afrika

    (GMT+08:00) 2017-11-16 18:37:07

    Wajumbe kutoka China, Ujerumani na Afrika wanaohudhuria mkutano wa 23 wa mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa UNFCCC mjini Bonn wamesema, kujenga mfumo wa ushirikiano wa pande hizo tatu kutasaidia kutimiza lengo la usimamizi wa hali ya hewa wa dunia nzima na kutimiza maendeleo endelevu. Kutokana na hali ya sasa, sekta ya nishati endelevu inaweza kuwa sekta ya majaribio ya kujenga mfumo huo, na uvumbuzi wa ujuzi, ujenzi wa uwezo na uanzishaji wa mashirika zinaweza kuwa mwelekeo wa ushirikiano.

    Jana ilikuwa siku ya Afrika ya mkutano wa Bonn, ambapo taasisi ya utafiti wa maendeleo ya Ujerumani na shirika la ushauri wa mambo ya China na Afrika zilifanya kongamano na kutoa jukwaa kwa wajumbe wa pande hizo tatu kujadili ushirikiano, kuhimiza ushirikiano wa kimataifa kwa wazo na mfumo zenye uvumbuzi, na kuharakisha kutimiza usimamizi wa hali ya hewa na maendeleo endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako