• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwekezaji wa China katika nchi za nje wapungua

    (GMT+08:00) 2017-11-16 18:48:01

    Ofisa mwandamizi wa idara ya ushirkiano ya wizara ya biashara ya China leo amesema, katika miezi 10 iliyopita ya mwaka huu, thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja wa China katika nchi za nje imefikia dola za kimarekani bilioni 86.31, na kupungua kwa asilimia 40.9 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Hali hii inatokana na hatua zilizochukuliwa na China za kuzuia uwekezaji ovyo katika nchi za nje. Baadaye China itachukua hatua zaidi kama hizo. Katika miezi 10 iliyopita ya mwaka huu, wawekezaji wa China wametoa uwekezaji wa moja kwa moja wa dola za kimarekani bilioni 86.31 katika nchi za nje, thamani hii imepungua kwa asilimia 40.9 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Ofisa mwandamizi wa idara ya ushirikiano ya wizara ya biashara ya China Bw. Han Yong amesema, ingawa uwekezaji wa China katika nchi za nje unapungua, lakini kasi ya kupungua inashuka, huku muundo wa uwekezaji huo ukiboreshwa. Anasema,

    "Kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, kasi ya kupungua kwa uwekezaji wa moja kwa moja wa China katika nchi za nje imeshuka kwa asilimia moja ikilinganishwa na robo tatu ya mwisho ya mwaka jana. uwekezaji huo umeingia sekta za ukodishaji, huduma za biashara, uzalishaji, mauzo ya jumla na ya rejareja, upashanaji habari, software na huduma za tekenolojia za habari. Hakukuwa na miradi mipya katika sekta za nyumba, michezo na burudani."

    Bw. Han Yong amesema, hivi sasa uwekezaji wa China katika nchi za nje unaendelea kwa utulivu na utaratibu, na uwekezaji kiholela unazuiliwa. Wakati huo huo, katika miezi 10 iliyopita ya mwaka huu, ushirikiano wa uwekezaji kati ya China na nchi zinazohusika kwenye pendekezo la "ukanda mmoja na njia moja" unaendelea kusukumwa mbele kwa utulivu, na uwekezaji wa kampuni za China katika nchi hizo umeongezeka kwa asilimia 4.7 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Ongezeko hili haswa linatokana na miradi mikubwa ya ushirikiano kati ya China na nchi hizo.

    Aidha, Bw. Han Yong amesema China itachukua hatua zaidi ili kuzuia uwekezaji kiholela katika nchi za nje.

    Naibu mkurugenzi wa idara ya habari ya kituo cha mawasiliano ya uchumi wa kimataifa cha China Bi Wang Xiaohong anaona kuwa, licha ya hatua za kuzuia uwekezaji kiholela, kupungua kwa uwekezaji wa China katika nchi za nje pia kunatokana na sababu nyingine, kama vile mazingira ya fedha na mabadiliko ya sera zinazohusika. Anasema,

    "China inapaswa kuboresha mazingira ya uwekezaji katika nchi za nje kwa kampuni zake katika nyanja mbalimbali, zikiwemo sera, fedha na ujenzi wa jukwaa la habari. Kwani kila nchi ina hali yake tofauti, na kampuni za China zitakabiliwa na changamoto kubwa zikikosa huduma za kupasha habari."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako