• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchunguzi umeanza kuhusu ajali ya ndege iliyoanguka Tanzania na kusababisha vifo vya watu 11

    (GMT+08:00) 2017-11-17 09:30:35

    Timu ya wataalamu wa uchunguzi wa ajali za ndege kutoka wizara ujenzi, usafirishaji na mawasiliano ya Tanzania imefika mjini Arusha kuchunguza chanzo cha ajali ya ndege ya watalii iliyoanguka katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro, na kusababisha vifo vya watu 11.

    Kaimu mkuu wa Idara ya uchunguzi wa ajali za ndege ya Tanzania Bw. Paul Kweka, amesema wataalamu wa idara hiyo wako tayari kukutana na wamiliki wa ndege hiyo, kampuni ya Coastal Aviation, kuanza uchunguzi wa chanzo cha ajali.

    Tayari mabaki ya ndege iliyoanguka yamepatikana, na miili ya watu waliokufa kwenye ajili hiyo imondolewa kutoka kwenye eneo la tukio.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako