• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Naibu rais wa Afrika Kusini ataka uchunguzi kuhusu "kashfa ya kutekwa kwa idara muhimu za serikali" ufanyike mara moja

    (GMT+08:00) 2017-11-17 10:11:09

    Naibu rais wa Afrika Kusini Bw. Cyril Ramaphosa Alhamisi alitaka tume ya mahakama inayoshughulikia uchunguzi kuhusu kashfa ya kutekwa kwa idara muhimu za serikali nchini humo iundwe mara moja.

    Bw. Ramaphosa amesema kuna ushahidi mwingi kuwa idara muhimu za serikali zinatekwa kwa ajili ya maslahi binafsi, na hali ya rasilimali za umma kuhamishiwa kwa familia kadhaa na watu binafsi bado inaendelea.

    Wakati alipoulizwa kuhusu msimamo wa rais Jacob Zuma, Bw. Ramaphosa amesema hakuna dalili kuwa Rais Zuma anapinga kuundwa kwa tume hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako