Mkuu wa kitengo cha utekelezaji wa miradi katika wizara ya vijana William Furaha pia amewataka vijana kutumia raslimali chache walizonazo kuanzisha biashara na pia kubuni bidhaa mpya.
Furaha aliyasema hayo kwenye hafla ya YouthConnekt Awards kuzawadi vijana wabunifu kwenye eneo la Kaskazini.
Mshindi wa tuzo hilo alikuwa ni Jean Paul Ntezimana, mwenye unmri wa miaka 26 anayezalisha mvinyo kwa kutumia viazi
Ntezimana anamiliki kampuni ya mvinyo ya Iyiwacu Wine inazozalisha pia biskuti na donati kwa kutumia viazi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |