• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kuimarisha vita dhidi ya dawa za kulevya

    (GMT+08:00) 2017-11-18 16:59:57

    Tanzania imerekebisha sheria ya kuiongezea madaraka Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) ili kudhibiti biashara ya dawa za kulevya.

    Marekebisho hayo yataruhusu DCEA kumiliki silaha na kutumia maofisa wenye silaha wakati wa kuwakamata wafanyabiashara wakubwa wa dawa hizo.

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ameliambia Bunge kuwa sheria iliyorekebishwa pia itaipa DCEA madaraka ya kufunga akaunti za benki za watuhumiwa wa biashara kubwa ya dawa za kulevya kwa muda maalum.

    Bibi Mhagama pia amesema DCEA itaweza kushughulikia kuingizwa na kumiliki kinyume cha sheria kemikali zinazozuiwa ambazo zinaweza kutumiwa katika kuzalisha heroin, cocaine na vifaa vya mlipuko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako