• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan na Marekani zaendelea kutatua masuala kati yao

    (GMT+08:00) 2017-11-19 16:24:25

    Ziara ya naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Sullivan nchini Sudan na mazungumzo yake na maofisa wa Sudan imeweza kuwa mwanzo wa awamu ya pili ya mpango wa kiujenzi wa kusuluhisha masuala kati ya nchi hizo mbili.

    Mazungumzo ya ndani kati ya waziri wa mambo ya nje ya Sudan Ibrahim Ghandour na Bw. Sullivan wakati wa ziara hiyo yalitoa nafasi ya kuanzisha njia mpya ya mazungumzo.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Sudan imesema, njia hiyo ni pamoja na kuliondoa jina la Sudan kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi, kulifuta deni la nchi hiyo, kuhakikisha kuwa Sudan inajiunga na Shirika la Biashara Duniani (WTO) na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.

    Kwa upande wake, Bw. Sullivan ameitaka serikali ya Sudan na makundi ya waasi kusitisha mapigano katika mikoa ya Kordofan Kusini, Blue Nile, na Darfur.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako