• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ngwini wanapenda kula viwavi wa baharini

  (GMT+08:00) 2017-11-20 16:46:30

  Viwavi wa baharini wana maji mengi na lishe chache, hivyo watu walikisia kuwa ngwini hawapendi kula viwavi. Kikundi cha watafiti wanaotoka idara mbalimbali ikiwemo taasisi ya ncha za dunia ya Japan zimefanya uchunguzi na kugundua kuwa ngwini wanawinda na kula viwavi mara kwa mara.

  Watafiti wameweka kamera ndogo kwenye miili ya ngwini 106 za aina nne, ili kuchunguza mienendo yao chini ya maji. Ngwini hao wanaishi katika sehemu mbalimbali duniani ikiwemo ncha ya kusini, Argentina na Australia. Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kuwa ngwini wanakula viwavi na viumbe wengine wanaofanana na jeli mara kwa mara. Watafiti wamepata picha zao za kuwawinda viwavi mara 200, na hata kulipokuwa na chakula kingine baharini, ndege hao bado wanawawinda viwavi.

  Ugunduzi huo umewafanya watu kufikiria tena mchango wa viumbe wanaofanana na jeli katika kutoa chakula baharini wakiwa ni chakula cha wanyama wakubwa wa baharini. Utafiti huo umetolewa kwenye gazeti la Frontiers in Ecology and the Environment la Marekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako