• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rasilimali mpya ya nguo inaweza kudumisha joto la wastani nguoni

  (GMT+08:00) 2017-11-20 16:46:50

  Wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Stanford wamesanifu rasilimali mpya ya nguo ambayo inaweza kurekebisha joto la nguo kwa mujibu wa mabadiliko ya hali ya hewa. Katika siku za joto, nguo inapunguza joto, na katika siku za baridi, nguo inapasha moto, na kuwafanya watu wahisi joto la wastani.

  Rasilimali hii mpya inafanana na karatasi ya kawaida ya alumini inayotumiwa jikoni. Wanasayansi wameweka matabaka mawili ya rasilimali inayopasha moto na tabaka la rasilimali inayopunguza joto. Tabaka la Polyethylene linalofunikwa na shaba linaweza kuvuta joto la ngozi, na matabaka ya Carbon yanaweza kutoa joto.

  Rasilimali hii ikishonwa kuwa nguo, na kulifanya tabaka la Polyethylene liwe nje katika majira ya baridi, nguo hii itavuta joto kutoka nje na kupasha moto ndani. Na katika majira ya joto, matabaka ya Carbon yatawekwa nje, nguo hii itatoa joto nje, na kupunguza joto la nguoni.

  Rasilimali hii imesanifiwa na kikundi cha watafiti wa kitivo cha sayansi na uhandisi wa rasilimali cha chuo hiki, na imefadhiliwa na idara ya utafiti ya wizara ya nishati ya Marekani. Watafiti wamesema ingawa rasilimali hiyo sasa bado haiwezi kutumiwa mara moja katika utengenezaji wa nguo, lakini ina mustakabali mzuri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako