• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya kuunda baraza la mawaziri la Ujerumani yashindwa

    (GMT+08:00) 2017-11-20 18:29:23

    Vyombo vya habari vya Ujerumani vimesema, chama cha LDP cha Ujerumani kimetangaza kujitoa kwenye majadiliano ya kuunda baraza la mawaziri.

    Mwenyekiti wa chama hicho amesema sababu ya kujitoa kwenye mazungumzo ni vyama vyote kutokuwa na uaminifu na umoja.

    Kiongozi wa chama cha Umoja ambaye pia ni waziri mkuu wa Ujerumani Bibi Angela Merkel amekilaumu chama cha LDP kwa kujitoa kwenye mazungumzo ya kuunda baraza la mawaziri.

    Mmoja wa viongozi wa Chama cha kijani amesema kuwa mazungumzo kati ya vyama yamepata maendeleo mazuri, na ni wajibu wa vyama vyote kuendelea na mazungumzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako