• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Spika wa Bunge la China akutana na rais wa Panama

    (GMT+08:00) 2017-11-20 18:35:38

    Spika wa bunge la umma la China Bw. Zhang Dejiang leo hapa Beijing amekutana na rais Juan Carlos Varela wa Panama.

    Bw. Zhang Dejiang amesema kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Panama kunaendana na maslahi ya kimsingi ya nchi hizo mbili na wananchi wao. Ameongeza kuwa rais Xi Jinping wa China na rais Varela walifanya mazungumzo muhimu, ambapo waliweka mpango mpya wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

    Rais Varela amesema Panama itashikilia sera ya kuwepo kwa China moja, na kwamba nchi yake inapenda kuimarisha ushirikiano na China kwenye sekta mbalimbali, pia anaunga mkono mawasiliano ya mabunge ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako