• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM asema tunawasikitisha watoto

    (GMT+08:00) 2017-11-21 14:38:26

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana ameeleza kusikitishwa na ukweli kwamba dunia inawakatisha tamaa watoto kwa kuwaacha wakabiliwe na hali ngumu na mateso.

    Bw. Guterres ameyasema hayo jana kwenye mkusanyiko wa watoto katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York ikiwa ni shughuli ya kuadhimisha Siku ya watoto duniani. Amesema mamilioni ya wasichana na wavulana wako hatarini, tunawakatisha tamaa, ambapo wanakimbia migogoro, wanakabiliwa na njaa, au kukosa dawa wanazohitaji, wanatengeka na wazazi wao, ama wako kwenye safari ndefu na yenye hatari kutafuta usalama, na kuishi katika kambi ya wakimbizi iliyoko mbali na nyumba zao.

    Ameongeza kuwa, hali hizo hazikubaliki kabisa. Umoja wa Mataifa ukiwa jumuiya ya kimataifa, hawawezi kuendelea kuwasikitisha watoto wote. Amesisitiza kuwa kila mtoto ana haki ya kuwa na maisha ya utoto yenye usalama, afya na amani na kuweza kuendeleza uwezo wao.

    Pia ameahidi kufanya juhudi zote kuhakikisha Umoja wa Mataifa unafanya kazi kwa ajili ya maslahi ya watoto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako