• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ayataka mashirika yasiyo ya kiserikali kando ya Njia ya Hariri kuimarisha ushirikiano

    (GMT+08:00) 2017-11-21 17:50:10

    Rais Xi Jinping wa China amesema mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO's) kando ya Njia ya Hariri yanapaswa kuchangia katika kuimarisha maelewano ya pamoja na urafiki kati ya watu wa nchi mbalimbali, kuboresha maendeleo ya pamoja, na kujenga jamii yenye hatma ya pamoja.

    Rais Xi amesema hayo kwenye barua yake ya pongezi kwa Kongamano la Kwanza la Ushirikiano wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Njia ya Hariri lililoanza leo hapa Beijing. Rais Xi amesema kujenga mtandao wa ushirikiano wa NGO katika Njia ya Hariri ni hatua muhimu kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati ya watu walioko kwenye Njia ya Hariri na kurahisisha maingiliano ya watu na watu.

    Zaidi ya mashirika 300 yasiyo ya kiserikali duniani yamejiunga na mtandao huo wa ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako