• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Maonyesho ya ujenzi wa nyumba kufunguliwa 22 Novemba Kigali

    (GMT+08:00) 2017-11-21 18:42:26

    Maonyesho ya ujenzi wa nyumba ya Afrika Mshariki Buildexpo Africa, yanatarajiwa kufunguliwa kesho mjini Kigali Rwanda.

    Maonyesho ya awali yalifanyika Kenya, Tanzania na Ethiopia kwa miaka 21 iliopita.

    Mkuu wa mawasiliano wa shirika la Expogroup ambalo linaandaa maonyesho hayo Asif Mavany, amesema mojawepo wa malengo ni kuionyesha Rwanda kwenye soko la kimataifa.

    Aidha amesema maonyesho hayo yataleta pamoja wadau kutoka zaidi ya nchi 20 kuonyesha teknolojia za kisasa na mashine za ujenzi wa nyumba.

    Mkurungezi wa halmshauri ya maendeleo nchini Rwanda Clare Akamanzi amesema maonyesho hayo yatasaidia kuitangaza Rwanda kama kituo bora kwa wawekezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako