• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: TFC kwa kushirikiana na kampuni ya ya China kuchimba visima

    (GMT+08:00) 2017-11-21 18:44:43

    Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) kwa kushirikiana na kampuni ya Juren Group ya China wanatarajia kuchimba visima virefu na mabwawa ili kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya umwagiliaji.

    Mbali na kuchimba visima na mabwawa hayo, kampuni hiyo ya Kichina itajenga kiwanda cha uunganishaji matrekta eneo Misugusugu mjini Kibaha ili kuinua sekta hiyo na kuimarisha kipato cha wananchi.

    Mkurugenzi wa ushirika na maendeleo, Henry Mwimbe alisema idadi ya visima na mabwawa yatakayochimbwa itafahamika baadaye lakini dhamira ya TFC ni kuhakikisha maisha ya wanachama wake yanaboreshwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako