• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Uchumi wa Tanzania miongoni mwa bora Afrika, yasema benki kuu

    (GMT+08:00) 2017-11-21 18:44:59

    Benki Kuu Tanzania (BoT) imesema, Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zenye viwango vya juu vya ukuaji wa uchumi katika kipindi cha muongo mmojauliopita (2007 - 2016).

    Mkurugenzi wa Uchumi BoT, Johnson Nyella amesema uchumi wa Tanzania ulikua kwa wastani wa asilimia 6.7 mwaka 2016, wakati pato la taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 7, sawa na ilivyokuwa mwaka 2015 na 2014.

    Nyella alisema hayo jana wakati wa sherehe ya Siku ya Takwimu Afrika (2017), iliyofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam.

    Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa Bot, kwa miaka minne mfululizo, mfumuko wa bei wa Taifa umeendelea kupungua na kubaki katika kiwango cha tarakimu moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako