• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mechi za leo za Michuano ya klabu bingwa Ulaya

    (GMT+08:00) 2017-11-22 10:29:25
    Michuano hiyo inaendelea usiku wa leo kwa mechi za raundi ya tano katika hatua ya makundi ambapo viwanja 8 vya miji tofauti barani Ulaya vitawaka moto, kukishuhudiwa timu za makundi A B C na D zikicheza.

    Katika kundi A, FC Basel wa Uswisi wanaikaribisha Manchester United, Benfica watakuwa wageni wa CSKA Moscow nchini Urusi, na kundi B Anderlecht ya Ubelgiji itacheza nyumbani dhidi ya Bayer Munich, huku PSG ya Ufaransa itacheza na Celtic ya Scotland.

    Kundi C ni FC Qarabag dhidi ya Chelsea, na atletico Madrid itacheza na AS Roma, na kundi D ni Juventus wakicheza na Barcelona, lakini Sporting Lisbon watawakaribisha Olympiakos nchini Ureno.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako