• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Mugabe wa Zimbabwe ajiuzulu

    (GMT+08:00) 2017-11-22 10:58:17

    Spika wa bunge la Zimbabwe Bw. Jacob Mudenda ametangaza kuwa, rais Robert Mugabe wa nchi hiyo amejiuzulu.

    Bw. Mudenda alisoma barua ya kujiuzulu ya rais Mugabe kwenye mkutano wa pamoja wa mabaraza mawili ya bunge la nchi hiyo. Amesema bunge la nchi hiyo litaweka njia ya kumchagua rais mpya kwa mujibu wa sheria.

    Katika barua yake ya kujiuzulu, Rais Mugabe alisema amejiuzulu kwa hiari, pia ana matumaini kuwa makabidhiano ya madaraka yatafanyika katika hali ya utulivu na amani.

    Baada ya kujiuzulu kwa rais Mugabe ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 37, viongozi wa Umoja wa Mataifa wametoa mwito kwa wazimbabwe wajizuie na kudumisha utulivu na amani nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako