• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umbo la sayari ndogo kutoka nje ya mfumo wa jua linafanana na sigara

  (GMT+08:00) 2017-11-22 15:56:24

  Darubini ya taasisi ya unajimu ya Chuo Kikuu cha Hawaii cha Marekani imegundua sayari ndogo ya kipekee mwezi uliopita. Sayari hii imepewa jina la Oumuamua, ambalo linamaanisha "mjumbe kutoka mbali" katika lugha ya Kihawaii. Hii ni mara ya kwanza kwa binadamu kugundua sayari inayotoka nje ya mfumo wa jua, na mwishowe sayari hiyo ikaondoka.

  Baada ya kugundua sayari hii, watafiti wameichunguza kupitia darubini mbalimbali zilizoko duniani kote. Uchunguzi unaonesha kuwa sayari hiyo inazungusha mara mmoja kila baada ya saa 7.3, na kiasi cha mwanga unaotolewa na sayari hiyo pia kinabadilika kwa mara 10. Hali hii haijawahi kutokea kwenye sayari ndogo au vimondo vya mfumo wa jua.

  Mnajimu wa taasisi hiyo Karen J. Meech amesema mabadiliko makubwa ya mwanga yanamaanisha kuwa sayari hii ni nyembamba sana, ambayo ina kipenyo cha mita 400, na urefu wake huenda ni mara 10 ya kipenyo chake.

  Idara ya anga ya juu ya Marekani NASA inasema tarehe 20 Novemba sayari hii ilikuwa umbali wa kilomita milioni 200 kutoka dunia, itapita mzingo wa Jupiter mwezi Mei mwakani, na itaondoka kwenye mzingo huo mwezi Januari mwaka 2019 na kuelekea kundi la nyota la Pegasus.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako