• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Robinho: Ahukumiwa kwenda jela miaka tisa

    (GMT+08:00) 2017-11-24 09:40:22
    Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Robson De Souza (Robinho) amehukumiwa kifungo cha miaka 9 jela baada ya kudaiwa kufanya tukio la ubakaji mwaka 2013 alipokuwa mjini nchini Italia akiitumikia klabu ya AC Milan.

    Robinho anadaiwa mbaka binti mwenye umri wa miaka 23 mwenye asili ya Albania na kisha kumtelekeza.

    Kwa mujibu wa sheria, mahakama ya Italia imempa nafasi kabla ya hukumu kuanza.

    Hii sio mara ya kwanza kwa Robinho kupatwa na kesi ya ubakaji kwani mwaka 2009 mshambuliaji huyo alikumbwa na kashfa kama hiyo baada ya kudaiwa kumbaka mwanafunzi wa chuo cha Leeds nchini Uingereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako