• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikosi cha nne cha askari wa miguu wa kulinda amani wa China chaanza kutelekeza majukumu Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2017-11-24 10:44:29

    Batalioni ya nne na ya tatu ya askari wa miguu wa kulinda amani wa China nchini Sudan Kusini jana zilifanya hafla ya kupokezana zamu katika kambi ya Umoja wa Mataifa huko Juba, kuashiria kuwa batalioni ya nne ya China imeanza rasmi kutekeleza majukumu yake nchini humo.

    Mkuu wa batalioni ya nne Bw Chen Ximing amesema operesheni za kulinda amani nje ya nchi ni jukumu kuu ililopewa na taifa, pia ni fursa ya kuonyesha sifa nzuri ya jeshi la China. Amesema batalioni yake itafanya juhudi zote katika kazi za kulinda amani nchini Sudan Kusini.

    Wakati huo huo ofisa wa Sudan Kusini amethibitisha kuwa mapambano yaliyoibuka tarehe 19 mwezi huu kati ya jeshi la serikali na kundi la waasi yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 25.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako