• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Semina ya mawasiliano ya elimu na ushirikiano wa kiviwanda kati ya China na Afrika wafanyika mjini Tianjin, China

    (GMT+08:00) 2017-11-24 16:36:17

    Semina ya siku mbili kuhusu mawasiliano ya elimu na ushirikiano wa kiviwanda kati ya China na Afrika ulioandaliwa na chuo kikuu cha ualimu cha ufundi stadi cha Tianjin na kamati ya Umoja wa Mataifa umefanyika leo mjini Tianjin, China. Wataalam zaidi ya 100 kutoka nchi 9 za Afrika na China wanajadiliana kuhusu maendeleo ya sekta ya viwanda na elimu ya nchi za Afrika, historia, hali ya sasa na mustakabali wa ushirikiano wa kiviwanda, mahitaji ya wataalamu wa mkakati wa ushirikiano wa kiviwanda kati ya China na Afrika na jinsi ya kuunganisha mikakati ya pande mbili. Fadhili Mpunji ana maelezo zaidi.

    Kwenye ufunguzi wa semina hiyo, Dk. Beatrice Njenga wa idara ya nguvukazi na teknolojia ya kamati ya Umoja wa Afrika, amesema kwa muda mrefu, China imetoa msaada mkubwa kwa maendeleo ya Afrika. Maendeleo ya kasi ya kiuchumi na kijamii ya China, si tu yameongeza nguvu ya taifa na ushawishi wa kimataifa wa China, na uzoefu wenye mafanikio uliopatikana kuhusu mtindo wa maendeleo wa China pia umetoa mfano wa kuigwa kwa nchi mbalimbali za Afrika. Hivi sasa, ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya China na Afrika unaendelea kuwa mzuri. Hivyo ni muhimu kwa wataalam wa nchi mbalimbali kushauriana jinsi ya kuongeza ushirikiano wa kiviwanda na uendelezaji wa nguvukazi kati ya pande hizo mbili, hatua ambayo itahimiza ushirikiano wa China na Afrika na utungaji sera ya maendeleo ya Umoja wa Afrika katika siku zijazo.

    Kwa upande wake, mkuu wa chuo kikuu cha ualimu cha ufundi stadi cha Tianjin Liu Xin amesema, ushirikiano wa kiviwanda ni sehemu muhimu katika pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na pia ni moja ya nguzo za uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na Afrika. Ushirikiano huo utasaidia China na Afrika kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja. Amesema, chuo hicho kitatumia vizuri fursa ya semina hiyo, kuendelea kusukuma mbele kazi za kituo cha utafiti wa mambo ya Umoja wa Afrika cha chuo hicho, kufundisha wanafunzi, kufanya utafiti wa kisayansi na kutoa huduma za kijamii ili kukiwezesha kituo hicho kiwe na uwezo wa kutoa mapendekezo kwa idara husika za kutunga sheria nchini China, na kutoa mchango zaidi kwa maendeleo ya ushirikiano na urafiki kati ya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako