• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Ofisi ya kuthibiti bei ya miraa kufunguliwa eneo la Maua Kenya

    (GMT+08:00) 2017-11-24 19:23:37
    Mkurungezi wa mamlaka ya kilimo nchini Kenya Alfred Busolo amesema wizara ya kilimo itaanza kuthibiti bei ya miraa ili kumlinda mkulima.

    Busolo amesema wanalenga kuondoa madalali wanaowapunja wakulima huku wakijipatia faida kubwa.

    Hapo kesho waziri wa kilimo Willy Bett anatarajiwa kufungua ofisi ya kushughulikia bei ya miraa katika mji wa maua kaunti ya Meru.

    Aidha Busolo amesema wanatafuta njia za kuuza miraa kwenye soko la kimataifa kupitia kwa uwanja wa ndege wa Isiolo badala ya kutumia ule wa Wilson mjini Nairobi ambao uko mbalo.

    Hata hivyo bado serikali inatafuta njia za kuanza tena kuuza miraa katika masoko ya ulaya ambayo tayari yalipiga marufuku bidhaa hiyo na kuiorodhesha kama dawa za kulevya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako