• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" la China na Tanzania lafanyika Beijing

    (GMT+08:00) 2017-11-24 19:25:56

    Kongamano la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kati ya China na Tanzania limefanyika kwenye ubalozi wa Tanzania nchini China.

    Wajumbe waliohuhudia kongamano hilo wamejadili kuhusu njia za kufanya ushirikiano kati ya China na Tanzania, kuanzisha jukwaa la kuzidisha uwekezaji wa biashara na kuhimiza uhusiano wa kusaidiana na kunufaishana wa pande hizo mbili.

    Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Tanzania Bw. Adolf Mkenda amesema, Tanzania ambayo ni nchi inayoshiriki kwenye pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na serikali inaboresha mazingira ya kiuchumi, ili kuwavutia zaidi wawekezaji wa China kuwekeza nchini Tanzania, na imepata maendeleo mazuri katika sekta hiyo.

    Naye Katibu Mkuu wa wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji ya Tanzania Bw. Elisante Ole Gabriel amesema, serikali ya Tanzania inatarajia kuinua ubora wa bidhaa za nchi hiyo kwa kupitia ushirikiano na China, ili kuwanufaisha watanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako