• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Jambojet kuanza kuhudumu Tanzania na Uganda mwezi Februari mwakani

    (GMT+08:00) 2017-11-27 18:17:15
    Shirika la ndege la Jambojet litaanza kuhudumu Tanzania na Uganda mwezi Februari mwaka ujao hiyo ikiwa ni sehemu yake ya kupanua oparesheni zake kufikia miji 16 mipya.

    Wizara ya uchukuzi imesema ilikuwa imetuma maombi ya kuhudumu kwenye nchi hizo.

    Aidha Jambojet ambayo ni tawi la shirika la ndege la Kenya Airways imeomba kupewa idhini kuhudumu Addis Ababa, Zanzibar, Kigali, Juba, Bujumbura, Hargeisa, Mogadishu, Goma, Kisangani na Moroni.

    Pia inapanga kuanza safari za mjini Wajir kaskazini mwa Kenya mwezi Februari mwaka ujao. Sasa shirika hilo linafanya safari katika miji ya Nairobi Mombasa, Eldoret, Kisumu, Lamu, Malindi na Ukunda (Diani).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako