• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatangaza wanataaluma wapya wa akademia ya sayansi

    (GMT+08:00) 2017-11-28 17:54:47

    Akademia ya sayansi ya China leo imetangaza matokeo rasmi ya uteuzi wa wanataaluma wapya, ambao ni pamoja na wachina 61 wakiwemo wanawake watatu na wengine 16 kutoka nchi za nje. Hii ni mara ya pili kwa akademia hiyo kuongeza wanataaluma tangu irekebishe mfumo wake wa uteuzi mwaka 2014. Mkuu wa akedemia hiyo Bw. Bai Chunli ameeleza matumaini yake kuwa, wanataaluma hao wapya watashikilia mawazo mazuri ya kiujuzi na kimaadili, na kuongoza kazi za utafiti wa sayansi, ili kuchangia maendeleo ya sayansi na teknolojia.

    Akademia ya sayansi ya China ilianza kazi ya kuwateua wanataaluma wapya tarehe mosi, Januari mwaka huu. Kwa kufuata utaratibu wa uteuzi wa mwanzo, tathmini ya awali, tangazo la majina ya watu walioteuliwa, tathmini ya mkutano na kura za maoni ya wanataaluma wote, watu 61 wamekuwa wanataaluma wapya rasmi. Halafu baada ya kura za maoni ya wanataaluma wote, watu 16 wameteuliwa kuwa wanataaluma wapya wenye uraia wa nchi za nje wa akademia hiyo, ambao miongoni mwao Profesa Andre K. Geim kutoka Uingereza na Profesa James Fraser Stoddat kutoka Marekani walipata tuzo ya Nobel.

    Habari zinasema wastani wa umri wa wanataaluma hao wapya ni miaka 54.1, na asilimia 91.8 wana umri chini ya miaka 60. Mtafiti wa taasisi ya utafiti wa kemikali na fizikia ya Dalian ya akademia ya sayansi ya China Bw. Zhang Donghui ni mmoja wa wanataaluma wapya wenye umri mdogo zaidi. Anatumai kusukuma mbele maendeleo ya utafiti wake.

    "Kutokana na maendeleo ya teknolojia ya kompyuta na mbinu nyingine za utafiti, umuhimu wa itikadi za kemikali unaongezeka siku hadi siku. Katika akademia ya sayansi ya China, wanataaluma wanaotafiti itikadi za kemikali ni wachache sana. Hivyo naona ninabeba majukumu makubwa."

    Bw. Guan Xiaohong ameshughulikia utafiti wa itikadi na matumizi ya mfumo wa miradi mikubwa. Anasema,

    "Utafiti ninaoshughulikia ni kuhusu uvumbuzi na uendelezaji wa miradi mikubwa ya miundo mbinu, nishati, umeme, mawasiliano ya barabarani na uzalishaji. Kuhakikisha miradi hiyo inaendelea kwa usalama ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi na ujenzi wa ulinzi wa taifa. Baada ya kuteuliwa kuwa mwanataaluma, napaswa kufanya kazi kwa bidii zaidi."

    Hii ni mara ya pili kwa akademia ya sayansi ya China kuwateua wanataaluma wapya tangu irekebishe mfumo wa uteuzi mwaka 2014, na inafuatiliwa sana na sekta ya sayansi na pande nyingine mbalimbali. Ili kuboresha mwundo wa wanataaluma, mwaka huu akademia ya sayansi ya China iliongeza uungaji mkono kwa sayansi mpya, ulinzi na nyanja nyingine za usalama wa taifa.

    Mkuu wa akademia ya sayansi ya China Bw. Bai Chunli ameeleza matumaini yake kuwa wanataaluma wapya watabeba majukumu ya kihistoria, na kuwa viongozi wa uvumbuzi wa sayansi, walimu wa vijana hodari na waenezaji wa moyo wa sayansi. Anasema,

    "Uanataaluma ni fahari kubwa, na maneno na vitendo vya wanataaluma vinafuatiliwa na watu wote. Hivyo tunapaswa kushikilia mawazo mazuri ya kiujuzi na kimaadili, na kuwa wanasayansi bingwa na watu wenye maadili."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako