• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Duru ya nane ya mazungumzo ya amani ya Geneva kuhusu suala la Syria yaanza

  (GMT+08:00) 2017-11-28 19:06:13

  Duru ya nane ya mazungumzo ya amani ya Geneva kuhusu suala la Syria inayoongozwa na Umoja wa Mataifa imeanza leo huko Geneva nchini Uswisi.

  Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Syria Bw. Staffan de Mistura amesema, kutunga katiba na kujadili uchaguzi mkuu wa Syria ni masuala muhimu ya mazungumzo hayo.

  Bw. De Mistura amesema, mchakato wa kisiasa wa suala la Syria unapaswa kufanyika kwenye msingi wa azimio namba 2254 la Umoja wa Mataifa, ambapo pande zote pia zitajadili ushirikiano wa kupambana na ugaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako