• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Juventus yazoa tuzo za Gran Gala del Calcio za ligi kuu ya Italia

    (GMT+08:00) 2017-11-29 09:07:35

    Timu ya Juventus imengára katika sherehe za utoaji wa tuzo za Gran Gala del Calcio za ligi kuu ya nchini Italia zilizofanyika mji wa Milan, kwa kuzoa tuzo nyingi zaidi. Timu hiyo imefanikiwa kushinda tuzo ya timu bora ya Italia baada ya kutwaa taji la ligi kuu ya nchi hiyo kwa mara sita mfululizo huku pia ikitoa wachezaji saba katika kikosi cha timu bora ya ligi ya Italia kwa mwaka 2016/17.

    Wakati huo huo kocha wa Napoli, Maurizio Sarri amefanikiwa kushinda tuzo ya kocha bora na golikipa wa Juventus, Gianluigi Buffon amefanikiwa kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa Serie A ambapo msimu uliopitta tuzo hiyo ilichukuliwa na Leonardo Bonucci.

    Wachezaji wengine ambao wametajwa kwenye kikosi hiko ni pamoja na Kalidou Koulibaly, Marek Hamsik, Dries Mertens (Wote kutoka Napoli), na Radja Nainggolan (AS Roma).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako