• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuadhimisha siku ya katiba

    (GMT+08:00) 2017-11-30 17:36:52

    China itaadhimisha siku ya nne ya katiba tarehe 4, Disemba. Hii pia ni mara ya kwanza kwa China kuadhimisha siku hiyo tangu kufanyika kwa mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC. Waziri wa sheria wa China Bw. Zhang Jun, ambaye pia ni mkurugenzi wa ofisi ya uenezi wa sheria ya China amesema, kauli mbiu ya siku hiyo kwa mwaka huu ni "kujifunza na kutekeleza maamuazi ya mkutano mkuu wa 19 wa CPC, na kulinda mamlaka ya katiba", na China inafanya kampeni ya uenezi katika sehemu mbalimbali nchini kuanzia mwishoni mwa Novemba hadi mwishoni mwa Disemba, ili kuhimiza watu wote kuheshimu, kujifunza, kufuata na kutegemea katiba.

    Siku ya katibu ambayo pia ni siku ya uenezi wa sheria ilianzishwa mwaka 2014, kwa lengo la kujenga uelewa kuhusu katiba, kueneza nia ya kufuata sheria, kuongeza nguvu ya kueneza sheria na kuhimiza watu kuheshimu, kujifunza, kufuata na kutegemea sheria. Kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa leo na ofisi ya habari ya baraza la serikali ya China, waziri wa sheria ya China Bw. Zhang Jun, ambaye pia ni mkurugenzi wa ofisi ya uenezi wa sheria ya China ameeleza mpango maalumu katika siku ya katiba kwa mwaka huu.

    "Ofisi ya uenezi wa sheria pamoja na mahakama kuu katikati ya mwezi Disemba zitawaagiza maofisa wa ngazi ya naibu waziri kutoka idara wanachama wa baraza la utaratibu wa majukumu ya kueneza sheria, wasikilize kesi za jinai mahakamani, ili watu hao wenye madaraka ya kutekeleza sheria wajue utaratibu wa mashtaka ya kesi."

    "Watu wanaotekeleza sheria kueneza sheria". Huu ni mpango muhimu uliobuniwa mwezi Mei mwaka huu na kikundi cha viongozi wa juhudi za kuzidisha mageuzi kwa pande zote cha kamati kuu ya CPC, kuhusu kazi ya kueneza sheria kwa watu wote nchini China. Hadi sasa kuna mikoa na miji 18 na idara 8 za serikali kuu zilizotoa njia ya kutekeleza mpango huo unaolenga kuchanganya uenezi wa sheria kwenye utekelezaji wa sheria. Bw. Zhang Jun anasema,

    "Zamani wafanyakazi wetu walipotekeleza sheria, walitangaza maamuzi tu bila ya kutoa maelezo mengi. Hali ambayo inaweza kudhuru maslahi ya watu husika na kusababisha ufujaji wa raslimali ya sheria. Sasa tunasisitiza 'Watu wanaotekeleza sheria waeneze sheria', maana yake ni watu wanaotoa uamuzi wa sheria wana majukumu ya kutoa maelezo kuhusu sheria husika."

    Kuhusu tukio la kuwadhuru watoto kwenye shule moja ya chekechea mjini Beijing, naibu waziri wa elimu wa China Bw. Tian Xuejun amesema, tukio hilo limetambulisha kuwa katika baadhi ya sehemu, bado sheria hazitekelezwi vizuri. Anasema,

    "Katika siku zijazo, wizara ya elimu itatunga hatua yenye nguvu zaidi ya usimamizi, na kukamilisha mfumo wa kuidhinisha walimu, pia tutafikiria kutunga nidhamu kwa ajili walimu, na kuwafahamisha kuhusu sheria husika. Aidha tutafanya uchunguzi kuhusu utungaji wa sheria ya elimu kwa watoto wadogo, ili kutoa uhakikisho wa sheria kwa shughuli za shule za chekechea."

    Bw. Tian Xuejun pia ameeleza kuwa vijana ni muhimu zaidi katika kazi ya uenezi wa sheria. Wizara ya elimu itachukua kutoa mafunzo ya sheria kwa vijana kama hatua muhimu ya kuwaelimisha. Hivi sasa wizara ya elimu kwa kushirikiana na wizara ya sheria zimetoa mwongozo wa juhudi za kuwafundisha vijana sheria, na kuanza vipindi vya maadili na sheria kwenye madarasa ya shule, na kuanzisha tovuti t na vituo vya uenezi wa sheria kwa vijana, ili kuhimiza juhudi hizo zipate ufanisi halisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako