• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa China kuhudhuria mkutano wa 16 wa mawaziri wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai

  (GMT+08:00) 2017-11-30 19:34:12

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amewasili Sochi, Russia, ambapo anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa 16 wa baraza la mawaziri wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai.

  Bw. Li Keqiang amesema tangu jumuiya hiyo ianzishwe miaka 16 iliyopita, imekuwa jukwaa muhimu la kulinda usalama na utulivu wa kikanda na kutimiza maendeleo na ustawi wa pamoja. Amesema anatarajia nchi wanachama wa jumuiya hiyo zitasukuma mbele ushirikiano katika mambo ya siasa, usalama, uchumi na utamaduni kwenye mwanzo mpya.

  Li Keqiang pia atazungumza na mwenzake wa Russia Bw. Dmitry Medvedev. Ameeleza matarajio yake kuwa mazungumzo hayo yataimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kuhimiza ushirikiano ndani ya jumuiya hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako