• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNAIDS yaishukuru China kwa Mchango wake katika kupambana na HIV barani Africa

    (GMT+08:00) 2017-12-01 15:34:40

    Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na Ukimwi UNAIDS, limesema China imekuwa mdau mkubwa na muhimu katika mapambano dhidi ya HIV na changamoto zake barani Afrika kutokana na kuimarika kwa ushirikiano uliopo baina China na mataifa ya Afrika.

    Akizungumza katika mahojiano maalum idhaa ya Kiswahili ya CRI kando ya mkutano wake na waandishi wa habari kwenye ofisi za makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Beijing, Mshauri Mwandamizi wa masuala ya Sera na Uratibu wa UNAIDS, Pride Chigwedere, amesema China imekuwa mstari wa mbele kuzalisha na kuuza dawa za kufubaza makali ya virusi vya Ukimwi ARVs, ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kulinda takribani watu milioni 21 kati ya milioni 26 walioathirika barani Afrika.

    Bw. Chigwedere ameongeza, UNAIDS sasa inafanya mazungumzo na makampuni kumi ya China yanayotengeza dawa ili yafungue viwanda kwenye Mataifa tofauti barani Afrika, ili kurahisisha upatikanaji wa tiba muhimu kwa wahitaji.

    "Ushirikiano baina ya China na Afrika ni kiwango cha juu kupitia jukwaa la maendeleo baina ya China na Afrika FOCAC na katika maazimio ya mwisho yaliyofikiwa kwenye mkutano wa mwisho uliofanyika nchini Afrika Kusini, na katika mkutano huo Rais Xi Jinping alipozungumza na marais hamsini wa nchi za Afrika, aliahidi kutoa dola bilioni 60 kwa ajili ya maendeleo ya ushirikiano huo, kiasi cha pesa ambacho ni kikubwa sana, na akiweka pia mipango kumi ya maendeleo, na moja ya mipango hiyo ni kuhusu afya ya jamii, hivyo kuna mpango wa kushirikiana katika kupigania za watu wa Afrika"

    Katika hatua nyingine, mwakilishi huyo wa UNAIDS amesema Mataifa ya Afrika yatanufaika na mipango mikubwa ya China ya kimaendeleo kwa nchi washirika wake, mmoja ikiwa ni program ya Belt and Road ambao Afya ya jamii ni miongoni mwa malengo yake.

    Lakini zaidi jukwaa la maendeleo baina ya China na Afrika FOCAC ambalo tayari limeanza kukushirikiana baadhi ya Mataifa ya Afrika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

    "pia kuna wataalam wa masuala ya Afya kutoka China ambao wamekuwa wakishiriki katika program mbalimbali za kimatibabu, na wengine wakitoa mafunzo kwa wafanayakazi wa sekta ya Afya barani Afrika, hivyo licha ya kutoa pesa nyingi, China imekuwa msaada mkubwa katika maendeleo ya uzalishaji wa dawa na vifaa tiba, mfano Kiwanda kikubwa cha kuzalisha dawa cha API ambacho ni miongoni mwa vikubwa duniani, hivyo nadhani kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa China na kufaidika pia kutokana na ushirikiano ambao natamani uimarike zaidi."

    Kuhusu takwimu za HIV barani Afrika, utafiti umeonyesha zaidi ya waathirika milioni 26 katika ya milioni 37 duniani wanapatikana, hivyo UNAIDS imeendelea kuwekeza nguvu zaidi kupambana na kutokomeza maambukizi, na kuboresha maisha ya wale walioathirika waishi muda mrefu.

    Kwa asilimia mia moja UNAIDS kwa kushirikiana na wadau wake, wamefanikiwa kuondoa tatizo la maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

    Huyu hapa tena Pride Chigwedere akifafanua takwimu hizoļ¼š

    ''Ripoti kuhusu ukimwi ya mwaka 2017 iliyotolewa novemba 20, kuna takribani watu milioni 37 wanaoishi na virusi vya ukimwi, na milioni 26 kati yao ni kutoka Afrika, kwa hiyo ukitazama Afrika pekee inachangia karibu asilimia sabini ya watu wenye maambukizi dunia nzima, kwa sababu athari ni kubwa zidi Afrika, hivyo hata jitihada za kupambana zimewekezwa zaidi huko, watu milioni 21 wenye maambukizi wanapata matibabu, na kati ya hao, takribani milioni 4 wanapatikana katika nchini Afrika Kusini pekee, kwa kuwa takwimu zinaonyesha kwamba Afrika Kusini ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya watu wenye maambukizi, zaidi ni kwamba karibia nusu ya wanaotumia dawa wapatao milioni 13 wapo barani Afrika."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako