• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idadi ya wahamiaji nchini Uingereza yapungua kwa kiasi kikubwa baada ya kufanyika kwa kura ya maoni kuhusu kujitoa EU

  (GMT+08:00) 2017-12-01 20:03:33

  Ofisi ya takwimu ya Uingereza imesema, ndani ya mwaka mmoja baada ya nchi hiyo kupiga kura ya maoni kuhusu kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, idadi ya wahamiaji nchini humo imepungua kwa zaidi ya laki moja na kufikia elfu 230, ikiwa ni kiasi kikubwa zaidi kupungua kwa mwaka tangu takwimu hizo zilipoanza kutangazwa.

  Takwimu hizo ni pengo kati ya watu waliohamia nchini Uingereza na waliohamia nchi nyingine kutoka Uingereza. Ofisa anayeshughulikia takwimu za wahamiaji Bi. Nicola White amesema, kwa jumla idadi ya watu waliohamia nchini Uingereza bado inazidi idadi ya watu waliohamia kwenye nchi nyingine kutoka Uingereza. Amesema kwa sasa ni vigumu kuthibitisha kama kupungua kwa takwimu hizo kutakuwa mwelekeo wa muda mrefu au la.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako