• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 4 wa mtandao wa internet duniani wafunguliwa

    (GMT+08:00) 2017-12-03 15:57:52

    Rais Xi Jinping wa China amepongeza mkutano wa nne wa mtandao wa internet duniani ambao umefunguliwa leo huko Wuzhen, mashariki mwa China.

    Kwenye salamu zake za pongezi, rais Xi ametoa wito kwa washiriki wote wa mkutano huo kutoa maoni yao, kuzidisha maelewano, kuimarisha ushirikiano kuhusu mtandao wa internet na uchumi wa kidijitali, ili mafanikio ya maendeleo yaliyopatikana kwenye sekta ya mtandao wa internet yawanufaishe vizuri watu wa nchi mbalimbali duniani. Rais Xi ameongeza kuwa mkutano mkuu wa 17 wa Chama cha Kikomunisti cha China uliomalizika hivi karibuni umepanga mpango wa utekelezaji wa maendeleo kuhusu ujamaa wenye umaalumu wa kichina katika enzi mpya, ambao umesisitiza kujenga China kuwa taifa la kidijitali lenye nguvu katika mtandao wa internet na na jamii yake kuwa ya kisasa, na kwamba China inatarajia kuwa nchi mbalimbali duniani zinanufaika kwa pamoja na maendeleo ya kasi ya mtandao wa internet na uchumi wa kidijitali na mlango wa China kwa nje hautafungwa kamwe.

    Afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Apple Tim Cook, baba wa internet Robert Kahn, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya Alibaba Jack Ma wametoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako