• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 13 wauawa na wengine 53 kujeruhiwa kufuatia mlipuko uliotokea sokoni nchini Nigeria

    (GMT+08:00) 2017-12-03 16:22:08

    Milipuko miwili iliyotokea sokoni katika mji wa Biu kaskazini magharibi mwa Nigeria siku ya jumamosi imeua watu 13 na wengine 53 kujeruhiwa.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa polisi Victor Isuku, wanawake wawili walikuwa na mabomu na kujitoa mhanga katika eneo lenye pilika sokoni humo lililopo kaskazini mwa jimbo la Borno.

    Polisi pia wanasema kundi la Boko Haram linahusika na shambulio hilo. Kundi hilo la kigaidi limeua jumla ya watu 20,000 nchini humo tangu mwaka 2009.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako