• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya awamu ya 10 ya vyama vya siasa vya China na Marekani yafanyika Beijing

    (GMT+08:00) 2017-12-04 19:13:18

    Mazungumzo ya awamu ya 10 ya vyama vya siasa vya China na Marekani yameanza leo hapa Beijing.

    Akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa mazungumzo hayo, mkuu wa idara ya mawasiliano na nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Bw. Song Tao amesema wanasiasa na wadau wa sekta ya mkakati kutoka China na Marekani wamekutana hapa Beijing, wakifanya majadiliano chini ya kauli mbiu ya "China na Marekani: mwanzo mpya, fursa mpya na ushirikiano mpya kati ya China na Marekani, katika msingi wa mfumo wa mkutano wa ngazi juu wa mazungumzo kati ya CPC na vyama vingine vya siasa duniani.

    Bw. Song ameongeza kuwa mazungumzo ya vyama vya siasa vya China na Marekani yatafanya kazi kwa nchi hizo mbili kutekeleza vizuri majukumu ya kusukuma mbele maendeleo ya dunia, kuendeleza uhusiano wa aina mpya wa nchi kubwa, kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja na kuhimiza ushirikiano wa kivitendo kati ya China na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako