Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amelaani shambulizi dhidi ya kituo cha ukaguzi cha polisi wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, ambapo askari mmoja wa kulinda amani ameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa.
Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric, amesema shambulizi hilo lilifanywa na wapiganaji wa anti-Balaka mjini Baria, na kusababisha kifo cha askari mmoja kutoka Mauritania.
Shambulizi hilo lilitokea saa mbili baada ya askari wa kulinda amani kuingilia kati kuwakomboa wakimbizi wawili waliotekwa nyara na wapiganaji wa anti-Balaka mjini Baria.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |