• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kwanini nyangumi wanakwama fukweni?

  (GMT+08:00) 2017-12-05 15:43:53

  Hivi karibuni nyangumi aina ya humpback alikwama mara mbili ufukweni huko Qidong, hapa China. Watu walijaribu kumwokoa lakini walishindwa. Kila mwaka nyangumi zaidi ya elfu moja wanakwama ufukweni, lakini wachache wanaokolewa.

  Nyangumi ana uwezo mdogo wa kuona, kwa kawaida anaweza kuona vitu vilivyoko ndani ya mita 17, uwezo huo mdogo hauendani kabisa na ukubwa wa nyangumi.

  Lakini nyangumi ana uwezo wa kutoa sauti aina ya Ultrasonic kama popo, sauti hii ikizuiliwa na kitu, inarudishwa. Nyangumi anathibitisha umbali kati yake na kitu mbele yake kupitia mwangwi.

  Wanasayansi wamekuwa wakijaribu kugundua sababu ya kukwama kwa nyangumi ufukweni, na kutoa maelezo mbalimbali, kwa mfano, mwangwi hausikiki vizuri kwenye ufukwe tambarare, mabadiliko ya ugasumaku yamewafanya nyangumi kushindwa kutambua upande, nyangumi wamepata ugonjwa wa vimelea, wameumwa kutokana na uchafuzi wa bahari, wamesumbuliwa na kelele zinazotoka kwenye sona, wanapowinda samaki wamekosea kuingia ufukweni, wanakwama wakati wanapotaka kuwaokoa wengine waliokwama, na wanataka kuishi kwenye nchi kavu kama vizazi vyao vya nyuma.

  Maelezo hayo yote hayawezi kueleza vizuri tabia za kukwama kwa nyangumi, na inaonekana kwamba wanasayansi bado wanahitaji kutafiti zaidi ili kupata jibu la swali hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako