• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Dalili ya maji kwenye sayari ya Mars huenda ni mtiririko wa mchanga tu

  (GMT+08:00) 2017-12-05 15:44:15

  Njia muhimu ya kutafuta viumbe kwenye sayari ya Mars ni kutafuta maji. Ushahidi uliwahi kuwafanya wanasayansi kuwa na matarajio makubwa ya kuwepo kwa maji kwenye Mars, lakini utafiti mpya umekanusha matarajio hayo.

  Kabla ya hapo, Idara ya anga ya juu ya Marekani NASA ilitangaza kugundua ushahidi unaothibitisha kuwepo kwa maji kwenye Mars, ambao ni michirizi myembamba iliyoko kwenye mteremko wa miamba. Milchirizi hiyo inatoweka katika majira ya baridi na kutokea tena katika majira ya joto. Baada ya kuchambua data za mwanga, wanasayansi wakakisia kuwa michirizi hiyo inatokana na mtiririko wa maji chumvi.

  Lakini hivi karibuni watafiti wa idara ya uchunguzi wa jiografia ya Marekani wamekanusha makadirio haya, wamesema huu huenda ni mtiririko wa mchanga, na sayari hiyo ina ukame na haifai maisha ya viumbe.

  Watafiti wamechambua michirizi 151 na kugundua kuwa mtiririko huo unafanana zaidi na mtiririko wa mchanga, kwani mtririko wa maji huwa ni mrefu zaidi na kwenda mahali pa chini zaidi.

  Wanasayansi waliwahi kutoa nadharia tete kwamba katika miaka bilioni 3 iliyopita kulikuwa na maji mengi kwenye Mars, lakini baadaye sayari hiyo ilibadilika kuwa kavu na baridi, na maji yaliganda na kulimbikizwa chini ya ardhi. Utafiti mpya umeunga mkono nadharia hii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako