• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa tatu wa UNEA wafungwa Nairobi

    (GMT+08:00) 2017-12-07 11:14:42

    Mkutano wa tatu wa siku tatu wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA ulifungwa jana mjini Nairobi, Kenya. Washiriki wa mkutano huo wametoa wito wa hatua za haraka na zenye uratibu kuchukuliwa kudhibiti uchafuzi na kuahidi kulinda afya ya binadamu na mazingira wanayoishi.

    Mkutano huo umetoa taarifa ya kwanza ya mawaziri wa mazingira, inayosema nchi mbalimbali zitaunga mkono juhudi za kudhibiti uchafuzi wa hewa, ardhi na maji unaodhuru afya ya binadamu, mfumo wa ikolojia na maendeleo ya uchumi.

    Mawaziri hao wameahidi kuongeza utafiti kwenye sekta ya mazingira, kuchukua hatua madhubuti katika kudhibiti uchafuzi, kuhimiza mtindo endelevu wa maisha na kuimarisha utungaji na utekelezaji wa sheria dhidi ya uchafuzi.

    Mkurugenzi wa UNEA Bw. Erik Solheim amesema, jambo muhimu kwa sasa ni kuhimiza utekelezaji wa kivitendo wa makubaliano yaliyofikiwa na kuleta mabadiliko halisi kwa maisha ya watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako