• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yarusha satelaiti ya mawasiliano ya Algeria

    (GMT+08:00) 2017-12-11 10:08:13

    China imerusha satelaiti ya kwanza ya mawasiliano ya Algeria "Alcomsat-1" kutoka kwenye kituo cha kurushia satelaiti cha Xichang mkoani Sichuan, kusini magharibi mwa China mapema leo.

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Algeria Bw. Abdelaziz Bouteflika wamepeana salamu za pongezi, wakipongeza kurushwa kwa mafanikio kwa saitelaiti hiyo.

    Kwenye salamu zake rais Xi amesema mradi wa satelaiti hiyo ni alama muhimu ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Algeria, na pia ni mfano wa mafanikio ya ushirikiano kati ya China na nchi za kiarabu kwenye sekta ya anga ya juu.

    Kwa upande wake rais Bouteflika amesema kurushwa kwa mafanikio kwa satelaiti hiyo ni mafanikio makubwa yaliyopatikana katika ushirikiano wa nchi hizo mbili kwenye sekta ya anga ya juu, na kuonesha urafiki mkubwa kati ya pande mbili.

    Satelaiti hiyo ikiwa ni mradi wa kwanza wa ushirikiano kwenye sekta ya anga ya juu kati ya nchi hizo mbili, itatumiwa na Algeria kwenye kurusha matangazo ya radio na televisheni, kuongoza mawasiliano ya barabarani, kufanya mawasiliano ya dharura na kujenga mtandao wa broadband.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako