• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka: Baada ya United Kufungwa, Kocha Guardiola amjibu Jose Mourinho

    (GMT+08:00) 2017-12-11 10:15:58

    Kama ilivyokuwa desturi yake, kocha mkuu wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amemlaumu mwamuzi wa mechi ya timu yake dhidi ya Manchester City, Michael Oliver, kuwa yeye ndiye aliyapelekea timu yake kufungwa.

    Mourinho amesema mwamuzi huyo aliinyima timu yake penati ya wazi ambayo ingesawazisha matokeo ya 2-1 yaliyoimaliza timu yake.

    Licha ya shutuma hizo kwa mwamuzi, Mourinho ametamka kuwa Man City wamepata kwa kuwa jana ilikuwa ni siku yao ya bahati.

    Kwa upande wake, kocha wa City, Pep Guardiola, amesema anaridhishwa na kiwango cha timu yake, na ndiyo maana wanapata ushindi.

    City sasa, wanafikisha alama 46 killeleni ikiwa ni 11 zaidi ya United walio katika nafasi ya pili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako