• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China, Russia na India zapaswa kuleta uhakikisho na hamasa zaidi kwa dunia

  (GMT+08:00) 2017-12-12 18:33:13

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema, China, Russia na India zimetambua jukumu lao la kimataifa, na zinapenda kuimarisha mawasiliano na uratibu, kutoa mchango kwa kutuliza hali ya kimataifa, na kuleta uhakikisho na hamasa zaidi kwa dunia.

  Bw. Wang Yi amesema hayo baada ya kukutana na wenzake wa Russia, na India huko New Delhi, India. Wang ameeleza sera ya kidiplomasia ya China katika kipindi kipya, akisisitiza kuwa China itatimiza ustawi kwa maendeleo ya amani. Pia amesema China, Russia na India zinapaswa kuelewana na kuigana, ili kupata maendeleo kwa pamoja. Pande hizo tatu zimekubaliana kuimarisha uhusiano kati yao, kupanua ushirikiano na kutoa mchango kwa amani na ustawi wa kikanda na dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako