• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Orodha ya wanasayansi wanaotunukiwa tuzo za mafanikio mkubwa ya sayansi za Marekani yatangazwa

  (GMT+08:00) 2017-12-13 08:58:15

  Orodha ya wanasayansi wanaotunukiwa tuzo za mafanikio mkubwa ya sayansi ya Marekani imetangazwa katika kituo cha utafiti cha Ames cha Idara ya anga ya juu ya Marekani NASA. Wanasayansi 12 duniani wamepata tuzo hiyo na watagawiwa dola za kimarekani milioni 21.

  Wanasayansi watano wakiwemo Joanne Chory kutoka taasisi ya biolojia ya Salk na taasisi ya matibabu ya Howard Hughes ya Marekani, Don Cleveland kutoka taasisi ya saratani ya Ludwig ya tawi la San Diego la Chuo Kikuu cha California Marekani, Kazutoshi Mori kutoka Chuo Kikuu cha Kyoto cha Japan, Kim Nasmyth kutoka Chuo Kikuu cha Oxford Uingereza na Peter Walter kutoka Chuo cha tawi la San Francisco la Chuo Kikuu cha California wamepewa tuzo za mafanikio makubwa ya biolojia.

  Chuck Bennett kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins Marekani, Gary Hinshaw kutoka Chuo Kikuu cha British Columbia Canada, Norman Jarosik kutoka Chuo Kikuu cha Princeton Marekani, David Spergel na Lyman Page wamepata tuzo za mafanikio makubwa ya fizikia ya msingi.

  Christopher Hacon kutoka Chuo Kikuu cha Utah na James McKernan kutoka tawi la San Diego la Chuo Kikuu cha California wamepata tuzo za hisabati.

  Tuzo za mafanikio makubwa ya sayansi za Marekani zilizoanzishwa mwaka 2012 ni tuzo zinazotoa fedha nyingi zaidi kwa washindi duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako