• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanajimu wagundua shimo jeusi kubwa lililoko mbali sana

  (GMT+08:00) 2017-12-13 08:59:26

  Kikundi cha kimataifa kimetoa ripoti kwenye gazeti la Nature la Uingereza ikisema kimegundua shimo jeusi kubwa lililoko mbali zaidi kuliko mashimo mengine yaliyogunduliwa, ambalo uzito wake ni mara milioni 800 ya jua.

  Kikundi hiki kimegundua shimo jeusi hili kwa kutumia satilaiti ya WISE ya Idara ya anga ya juu ya Marekani NASA na darubini ya Magellan iliyoko nchini Chile.

  Quasar ni galaksi maalum inayoundwa na shimo jeusi na vumbi na hewa. Shimo jeusi linapovuta vitu vilivyoko karibu, linatoa nishati nyingi na kuifanya quasar kung'ara.

  Uchambuzi unaonesha kuwa mwanga wa quasar hii ulifika duniani kwa kusafiri zaidi ya miaka bilioni 13, hii inamaanisha kuwa imekuwepo katika kipindi cha mwanzo baada ya ulimwengu kuundwa. Jinsi ulimwengu wa mwanzoni ulivyoweza kuunda shimo jeusi kubwa kama hili ni swali gumu ambalo haliwezi kujibiwa kwa kutumia nadharia za sasa kuhusu shimo jeusi.

  Wanasayansi wanakisia kuwa kuna quasar 20 hadi 100 zenye historia ndefu kama quasar hii ulimwenguni, na wanatarajia kugundua quasar nyingi zaidi ili kutafiti mabadiliko ya ulimwengu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako