• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya Nanjing yafanyika

    (GMT+08:00) 2017-12-13 11:16:16

    Maadhimisho ya kitaifa ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya halaiki ya Nanjing yamefanyika leo na kuhudhuriwa na rais Xi Jinping wa China.

    Huu ni mwaka wa 80 baada ya kutokea kwa mauaji ya Nanjing. Tarehe 13, Disemba mwaka 1937, wanajeshi wa Japani walivamia China na kuingia mjini Nanjing, na kufanya mauaji ya kimbari kwa siku zaidi ya 40. Kwa mujibu wa hukumu na uchunguzi uliofanywa na Mahakama ya Kijeshi ya Kimataifa ya Mashariki ya Mbali na Mahakama ya Kijeshi ya Nanjing, raia wa China na wafungwa wa vita laki tatu waliuawa na jeshi la Japani, wanawake elfu 20 wa China walibakwa na wanajeshi wa Japani, theluthi moja ya ardhi za mji wa Nanjing ziliteketezwa kwa moto na jeshi la Japani na uharibifu wa mali hauwezi kuhesabiwa.

    Mwaka 2014, Februari, bunge la umma la China lilipitisha sheria ya kufanya siku ya tarehe 13, Disemba kuwa siku ya kitaifa ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya halaiki ya Nanjing.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako