• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Maonyesho ya kibiashara ya China na Afrika yafunguliwa Nairobi

    (GMT+08:00) 2017-12-13 19:31:00

    Maonyesho ya kibiashara ya siku nne kati ya China na Afrika yamefunguliwa rasmi leo kwenye ukumbi ya KICC jijini Nairobi.

    Kampuni mbali mbali za Kichina zilizo hapa, zitatumia fursa hii ya kipekee kuwafikia wateja wengi, kando na kupokea maoni ya wateja hao kuhusu kampuni hizi na bidhaa zao.

    Ni mara ya kwanza kwa maonyesho hayo kuandaliwa barani Afrika na yanafuatia azimio la China la kuongeza uwezo Afrika wa kiviwanda lililofikiwa wkati wa mkutano wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika mjini Johannesburg mwaka 2015

    Maonyesho hayo yanaleta pamoja zaidi ya makapuni 56 makubwa kutoka mikoa 18 ya China manispaa mbali mbali.

    Pia miongoni mwa makampuni hayo ni 500 yalio makubwa zaidi nchini china kutoka shirika la kawi la kitaifa, shirika la ujenzi la china , China Telecom, China Unicom, shirika la nyuklia la China na beni ya kitaifa ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako