• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Duka la Nakumatt lafungwa Moshi

    (GMT+08:00) 2017-12-13 19:33:32

    Duka la Nakumatt limesalia na tawi moja tu nchini Tanzania baada ya duka lake la mjini Moshi kufungwa kwa kukosa kulipa kodi ya nyumba kwa mwaka mmoja.

    Haijabainika ni kiasi gani cha pesa lilalodaiwa duka hilo lakini lilifungwa ijumaa.

    Hilo ni duka la tatu la Nakumatt kufunguwa nchini Tanzania na sasa limesalia moja tu katika mji mkuu Dar es Salaam.

    Meneja wa jumba lililofungwa Moshi Thadey Mariki, amesema hawakuwa na budi kufunga tawi hilo kutokana na deni kubwa na pia athari mbaya kwa biashara yao.

    Nakumatt imekuwa ikikabiliwa na matatizo ya kifedha hali iliopelekea kufungwa kwa matawi yake mengi na pia kufutwa kwa wafanyakazi wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako