• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wavuvi mwanza watafuta wanunuzi wa dagaa

    (GMT+08:00) 2017-12-13 19:33:56

    Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Zambia, Malawi na Uganda zimetakiwa kujitokeza kununua samaki aina ya dagaa waliofurika katika Soko la Samaki Kirumba Mwaloni, jijini Mwanza.

    Ziwa Victoria lipo katika nchi tatu za Tanzania, Kenya na Uganda, lakini Tanzania ikiwa na eneo kubwa la ziwa hilo, asilimia 49.

    Mwenyekiti wa soko hilo, Fikiri Magafu amesema wateja wao wengine wakuu ni kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania kama vile Dar es Salaam, Mtwara na Pwani.

    Kwa mujibu wa Magafu, dagaa na samaki wengine wakiwamo aina ya sangara wanaovuliwa katika Ziwa Victoria wameongezeka sokoni hapo tangu Novemba mwaka huu kutokana na ongezeko la maji ziwani kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha.

    Hata hivyo, alielezea kuridhishwa na mahudhurio ya wafanyabiashara kutoka DRC akisema wamejitokeza saba katika kipindi cha wiki mbili na kwamba kila mmoja ameweza kununua magunia kati ya 100 na 1,000 yenye dagaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako