• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watafiti wachunguza papa nyangumi kwa mujibu wa madoa yao ya nyuma

  (GMT+08:00) 2017-12-14 09:15:09

  Kikundi cha watafiti cha kimataifa kimetafiti picha za papa nyangumi zilizopigwa na watalii kote duniani kwa miaka 22 na kugundua makazi ya papa nyangumi.

  Papa nyangumi ni samaki mkubwa zaidi duniani. Kila papa nyangumi ana madoa ya kipekee ambayo hayabadiliki kwenye sehemu zao za nyuma. Watafiti kutoka idara mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu cha Murdoch cha Australia wametoa ripoti kwenye gazeti la BioScience la Marekani ikisema wamerekebisha njia ya kutambua nyota iliyovumbuliwa na NASA na kuitumia njia hii kutambua papa nyangumi.

  Watafiti walikusanya picha zaidi ya elfu 30 za papa nyangumi zilizopigwa na watalii kote duniani, baada ya kuchambua picha hizi, wamefanikiwa kutambua papa nyangumi 6,000, na kugundua makazi mapya 7 ya papa nyangumi.

  Papa nyangumi wana urefu wa mita 10, lakini ni samaki wapole, ambao wanakula viumbe vinavyoelea baharini na samaki wadogo. Kutokana na uvuvi katika miaka 75 iliyopita, idadi ya papa nyangumi imepungua kwa asilimia 50 duniani, na wamewekwa kwenye orodha ya wanyama walio hatarini kutoweka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako