• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Atomu za Hydrogen duniani zinaweza kufika anga ya juu yenye umbali wa kilomita laki 2.4 kutoka dunia

  (GMT+08:00) 2017-12-14 09:15:29

  Watafiti wa Japan wamegundua kuwa atomu za Hydrogen duniani zinaweza kufika anga ya juu yenye umbali wa kilomita laki 2.4 kutoka dunia, ambao ni asilimia 60 ya umbali kati ya dunia na mwezi.

  Atomu za Hydrogen zinatokana na kuvujika kwa molekuli za maji chini ya mwanga aina ya UV. Mwaka 1972, wanaanga wa Marekani walipofika mwezini waliwahi kuchunguza atomu za Hydrogen zilizoko kando ya dunia, lakini wakati huo watu hawakujua atomu hizi zinasafiri kwa umbali gani kutoka dunia.

  Watafiti wa Chuo Kikuu cha Rikkyo cha Japan hivi karibuni walitoa ripoti kwenye gazeti la Geophysical Research Letters la Marekani ikisema wamepiga picha za hewa ya dunia iliyoko katika anga ya juu ambayo inaundwa na atomu za Hydrogen na Helium kwa kutumia darubini iliyoko kwenye chombo cha uchunguzi wa anga ya juu iliyorushwa na Japan mwaka 2014 ambayo iko kwenye umbali wa kilomita milioni 1.5 kutoka dunia, na kugundua kuwa atomu za Hydrogen za dunia zimefika anga ya juu yenye umbali wa kilomita laki 2.4 kutoka dunia.

  Watafiti pia wamegundua kuwa Atomu za Hydrogen zinatapakaa sawasawa kando ya dunia, na haziathiriwi sana na ugasumaku wa dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako